Hebrews 2:11-16

11 aYeye awafanyaye watu kuwa watakatifu, pamoja na hao ambao hufanywa watakatifu, wote hutoka katika jamaa moja. Hivyo Isa haoni aibu kuwaita ndugu zake. 12 bYeye husema, “Nitalitangaza jina lako kwa ndugu zangu;
mbele ya kusanyiko nitaimba sifa zako.”

13 cTena, “Nitaweka tumaini langu kwake.”

Tena anasema, “Niko hapa, pamoja na watoto ambao Mungu amenipa.”

14 dBasi kwa kuwa watoto wana nyama na damu, yeye pia alishiriki katika ubinadamu wao, ili kwa kifo chake, apate kumwangamiza huyo mwenye nguvu za mauti, yaani ibilisi, 15 ena kuwaweka huru wale waliokuwa utumwani maisha yao yote kwa sababu ya kuogopa mauti. 16 fKwa kuwa ni dhahiri kwamba hakuja kusaidia malaika, bali uzao wa Ibrahimu.
Copyright information for SwhKC